About Us

Chuo cha mtakatifu gaspar kilianzishwa mwaka 1988 na Padre Dominico Alteri wa shirika la wamisionari wa damu ya Azizi ya yesu aliyekuwa paroko mwaka huo akishirikiana na viongozi wa shirika la jimbo.

Lengo la chuo lilikuwa kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana na kuwasaida wejitegemee. kutokana na michango mbalimbali kutoka shirikani na kwa wafadhili mbalimbali chuo kimekuwa kikipiga hatua kubwa ya maendeleo kila mwaka. fani ya Ushonaji ndio ilikuwa ya kwanza kabisa chuoni na badae ziliongezwa fani nyingine kama Useremala,Uungaji vyuma,Umeme na Computer

Ilipofika mwaka 1995 chuo kilisajiliwa na VETA kikapewa namba ya usajili VTC 158/95. Mwaka 2010 usajili wa vyuo karibu vyote vya ufundi ulifutwa na mwaka 2012 chuo chetu kilipewa usajili wa mda namba VET/DSM/PR/2012/C/029. Na kwa sas tumepewa usajili wa kudumu wa namba VET/DSM/FR/2020/C/144.

Tangu mwaka 1995 chuo cha mtakatifu gaspar kimekuwa kikiboresha utoaji wake wa elimu na fani mbalimbali zimekuwa zikiongezeka pamoja na idadi ya wanafunzi. Na kwa sasa chuo kina fani zifuatazo Ushonaji (tailoring and design), Umeme (Electrical installation), Ufundi magari (Motor vehicle and Mechanics), Hotel management,Useremala (carpentry and joinery),Computer application, TEHAMA (information technology(IT)),beuty and hair dressing(salon), na Udereva wa magari madogo madogo. mpaka sasa tuna zaidi ya wanafunzi 300.

Our Achievements

KITAALUMA

kitaaluma tumekuwa na mafanikio makubwa kwa upande wa ufundi kwa wanafunzi wengi kufaulu mitihani ya ndani na mitihani ya taifa ya ufundi VETA

Pia kutokana na umakini wa walimu katika kuwaanda wanachuo, chuo chetu kimekuwa na sifa ya kuandaa vijana walioiva katika fani zao ambapo wengi wamejiajiri na wengine wameajiliwa na wanafanya vizuri sana.

Our Team


Padre Makarius

Padre Makarius

principal
madame kiwale

madame kiwale

deputy principal
madame stella

madame stella

Academic mistress
madame cessy

madame cessy

accounts